MOHAMED
Hussein, Mmachinga, mshambuliaji wa zamani wa timu ya Yanga na timu ya Taifa
amesema kuwa kikwazo kikubwa kwa mshambuliaji wa Yanga, David
Molinga ni ubonge wake tu ila kiuwezo yupo vizuri.
Molinga
ndani ya dakika ya 270 ambazo ni sawa na mechi tatu ametupia jumla ya mabao
mawili, ambapo moja alipachika kwa kichwa na lingine kwa mpira uliokufa kwenye
mchezo mmoja dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mmachinga amesema kuwa amemfuatilia kwa ukaribu Molinga na
kugundua kuwa ubonge wake unampa uzito wa kufanya maamuzi akiwa ndani ya
uwanja.
“Molinga ana
sifa za ushambuliaji hasa pale anapoamua kucheza namba tisa analijua lango na
ana uchu wa kufunga ila tatizo lake lipo kwenye uzito anashindwa kuwa na maamuzi
ya haraka kwake kila kitu ni kizito.
“Anajipa
majukumu mengi akiwa uwanjani kiasi kwamba unashindwa kujua anacheza namba
ngapi muda mwingine unamkuta yupo kwenye namba 10 wakati mwingine nyuma sasa
hapo kama ataendelea itampa wakati mgumu kufikia malengo, lakini akitulia na
asipopata majeruhi atafunga mabao mengi,” amesema Mmachinga.
0 COMMENTS:
Post a Comment