ABDALLA Mahmoud El Said Bekhit ni nyota wa timu ya Pyramids ya Misri ambaye ndiye tegemeo katika kikosi hicho kitakachomenyana na Yanga, Oktoba 27.
CCM Kirumba itawaka Moto kwa mchezo wa kwanza wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji ila anapewa jukumu la ushambuliaji ndani ya kosi hilo la Waarabu.
Huu ni msimu wake wa pili kucheza ndani ya kikosi hicho kitakachokuja Bongo hivi karibuni.
Ameletwa duniani mwaka 1985 kwa sasa ana umri wa miaka 34 alijiunga na Pyramids akitokea klabu ya Al-Ahli.
Uwezo wake mkubwa umejificha kwenye mguu wake wa kulia huku akiwa ni mbaya Kwa mipira iliyokufa na mjanjamja akiwa ndani ya 18.








0 COMMENTS:
Post a Comment