October 25, 2019


Waarabu wameumia! Ndivyo wanavyosema benchi la ufundi la Yanga lililo chini ya Mkongomani Mwinyi Zahera baada ya kuweka bayana kuwa wanazo taarifa zote muhimu juu ya wapinzani wao, Pyramids ya Misri.

Yanga ambao wana morali nzuri baada ya kushinda mechi zao mbili za Ligi Kuu Bara watakuwa wenyeji wa Pyramids katika mchezo wa kuwania nafasi ya kutinga Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, keshokutwa Jumapili.

Mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na Wanayanga wa Mwanza, itapigwa jijini humo katika Uwanja wa CCM Kirumba huku kiingilio cha chini kikiwa elfu saba za Kitanzania.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila raia wa Zambia ameliambia Championi Ijumaa, kuwa tayari wamepata taarifa zote muhimu kutoka kwa wapinzani wao ambazo walikuwa wanazitaka baada ya kuwafuatilia kwa kina.

“Huu ni mchezo muhimu kwetu kama ambavyo tumekuwa tukiipa umuhimu michezo yote ambayo tunacheza iwe ligi au michuano hii ya kimataifa. Tunajua nini tunakitaka na tukifanye kwa namna gani.

“Uzuri ni kwamba tumepata taarifa za wapinzani wetu na tutazitumia kwa ajili ya kuwamaliza siku hiyo, kitu cha msingi sisi kuendelea na mazoezi yetu lakini pia kuwa wamoja kwa ajili ya kushinda.

“Suala la kwamba tumewaona au hatujawaona hatuwezi kuweka wazi kwa sababu inabaki kama siri ya benchi la ufundi ila kitu cha msingi ni kuwa wachezaji wetu wanajiamini kwa sababu ya kushinda mechi zetu mbili zilizopita za ligi kuu mbele ya Coastal Union na Mbao FC,” alimaliza Mwandila ambaye aliletwa nchini na kocha George Lwandamina.

1 COMMENTS:

  1. Ishu co kuwaona dunia ya leo unazungumzia kuwaona ishu mmewaandaa vp wachezaji wenu kimbinu na kisaikoloji kuwakabili wapinzani wenu nyie vyura fc

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic