October 12, 2019






Na Saleh Ally
PAMOJA na mambo mengi sana, Bara la Ulaya ni maarufu kwa mchezo wa soka. Nchi mbalimbali zimejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo.


Kuna zile zimekuwa maarufu zaidi kupitia ligi za soka za nchi hizo. Mfano England kupitia Premier League, Ujerumani na Bundesliga, Hispania na La Liga au Ufaransa na Ligue 1 kama ilivyo Serie A kwa Italia.


Umaarufu huo unaendana na namna ushindani ulivyo, umaarufu wa klabu kadhaa na kadhalika. Lakini raha zaidi inapofikia michuano ya Ulaya kwa nchi, utaona utamu na ubabe wa zile nchi maarufu.


Kuna nchi ambazo hazijulikani kabisa, unapofikia wakati wa kuwania kucheza michuano ya Uefa European Championship Qualifying maarufu kama Euro, ndipo utaanza kuona ubabe wa baadhi za nchi unavyobadilika.


Babe unabadilika kwa kuwa timu ambazo hufanya vizuri zaidi mara nyingi zinakuwa si zile zenye ligi kubwa kama England na wale wanaoshuhudia michuano hiyo kupitia king’amuzi cha StarTimes, wanaweza kuwa mashuhuda.


StarTimes huonyesha mechi zote za michuano hiyo kwa ubora wa juu kabisa na kuwafikishia Watanzania wapenda mpira.


Uzuri wa michuano hiyo hufanyika wakati wa kipindi ambacho ligi zote za nchi katika Bara la Ulaya husimama na utaona wachezaji wanakuwa katika mwonekano mwingine.


Wachezaji wengi ambao wamezoeleka kuonekana mfano na jezi za Bayern Munich, PSG, Arsenal, Madrid wanakuwa katika mwonekano wa nchi zao.


Utawaona wanacheza na watu wengine si wale uliwazoea na huku burudani inakuwa tofauti kabisa. Na kuna baadhi ya timu zinakuwa na nguvu kubwa sana ukilinganisha na zile maarufu kutokana na ligi zao.


Ubelgiji haina ligi maarufu sana, kama unakumbuka Mtanzania Mbwana Samatta anacheza huko, lakini inapofikia timu ya taifa, wanakuwa na wachezaji nyota na mahiri wanaocheza katika Bundesliga, Ligue 1, Premier League, Serie A na kadhalika.


Hivyo, hii unaifanya timu yao kuwa imara zaidi na mfano mzuri ni mechi yao iliyopita dhidi ya San marino ambayo wameitwanga kwa mabao 9-0.


Mara ya mwisho, Ureno chini ya Cristiano Ronaldo waliitwanga Lithuania kwa mabao 5-1, Uturuki wakaiangusha Maldova kwa mabao 4-0, England wakatoa kipigo cha 5-3 kwa Kosovo ambao kidogo wakomae.


Uholanzi wakaiangusha Estonia kwa mabao 4-0 kama ilivyokuwa kwa Uswisi waliotoa kipigo kama hicho kwa Gibraltar.


Michuano hii ya Euro Qualify inakuwa ni sawa na mchujo wa kuwaondoa wadhaifu ili kupate imara kamili kwa ajili ya kwenda kushiriki michuano yenyewe.


Safari hii, Euro 2020 itafanyika katika miji 12 ya nchi 12 za Ulaya na itaanza Juni 12 hadi Julai 12, 2020.


Mfumo huu umekuwa na mvuto sana, wengi wangependa kuona aina mpya hiyo ya uendeshaji wa michuano katika nchi 12 kwa wakati mmoja.

Inasubiriwa kwa hamu sana kutokana na mfumo huo mpya na kila upande unataka kuwa mabingwa wa kwanza wa kihistoria tokea ifanyike kwa mfumo huo.

Hii pia utaona imechangia kwa kiasi kikubwa aina timu zilizoonekana hazitaweza kuibuka na kupambana ili ziingie katika kuwa za kwanza kushiriki katika michuano hiyo.

Mechi nyingi za michuano hiyo hasa kuwania kucheza Euro 2020, zitakupa picha kamili ya soka la Ulaya kwa kuwa unapata nafasi ya kuwaona wachezaji wakiwa na timu zao za taifa na si klabu kama ulivyozoea.



Kupitia StarTimes utaipata nafasi hiyo na utaona namna mchezaji uliyemzoea katika Bundesliga au Premier League anavyokuwa tofauti akiwa na kikosi cha Ubelgiji, Ujerumani au England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic