October 10, 2019


Manchester United wameafikiana makubaliano ya maongezi ya kumsajili mwezi Januari mshambuliaji wa Croatia na klabu ya Juventus Mario Mandzukic, 33. (Tuttosport, via Mirror)

Lyon wameshindwa mipango yao ya kumsajili kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho. Kocha huyo mwenye mika 56 raia wa Ureno anataka kurejea kwenye ligi ya Primia ya England. (Mirror)

Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki inaaminika kuanza mazungumzo na Arsenal juu ya kumsajili kwa mkopo mwezi Januari kiungo Mesut Ozil, 30. (Takvim, via Sun)

Mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller, 30, hana furaha baada ya kupunguziwa muda wa kucheza katika klabu yake ya Bayern Munich na amekiri kuwa anaweza kusaka timu ya kuhamia mwezia Januari. (Kicker, via Mail)

Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, na beki wa Brazil Thiago Silva, 35, wanaweza kuondoka bure kutoka klabu ya Paris St-Germain mwishoni mwa msimu. (ESPN)

Kiungo wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 31, ambaye alikuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Manchester United msimu uliopita, amesema kuwa huenda akaihama klabu yake ili kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza. (Mail)

Leeds wanapanga kumsajili kocha wa Rangers ya Uskochi Steven Gerrard endapo kocha wao Marcelo Bielsaataihama klabu. (Football Insider)

Manchester United wanapanga kumsajili kiungo Francisco Sebastian Cordova, ambaye anachezea klabu ya America ya Ligi Kuu nchini Mexico. Kiungo huyo mwenye miaka 22 ambaye ameichezea timu ya taifa lake kwa mara ya kwanza juma lililopita pia anatakiwa na Sevilla na Benfica. (Mail)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic