October 10, 2019


Beki wa kati wa Yanga, Andrew Vicent ‘Dante’ ameendelea na msimamo wake na safari hii amekataa kulipwa kwa mafungu madai yake ya Sh Mil. 40 anazodai.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassani Bumbuli alisema kuwa uongozi wa Yanga upo tayari kumlipa kwa mafungu kwa awamu tatu mfululizo, lakini yeye ameonekana kukataa.

Bumbuli alisema kuwa beki huyo anataka kulipwa fedha zote, hali ambayo uongozi unashangaa kwa kukataa fedha hizo ambazo wamepanga kumtangulizia Sh Mil. 15 atakazolipwa mara mbili na baadaye kumaliziwa Sh Mil. 10.

“Dante anachotakiwa kufahamu kuwa siyo mchezajji pekee anayedai Yanga wapo wengi na wote wamekubaliana kulipwa kwa awamu kama ilivyokua kwa Abdul (Juma) ambaye yeye tayari amejiunga na timu,”alisema Bumbuli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic