MAN UNITED YAZIDI KUMEGWA, MWINGINE KWENDA ITALY
Kiungo wa kati Manchester United na Serbia Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, anatafutwa na Inter Milan. (Sun)
Kiungo wa kati wa Barcelona Ivan Rakitic, mwenye umri wa miaka 31, ameacha azma yake ya kuhamia Manchester United mwezi Januari kwasababu Wacroasia hawataki ahamie Manchester. (Mail)
La Liga imependekeza kwa shirikisho la soka la Uhispania kwamba shindano la El Clasico lililiyopangwa tarehe 26 Oktoba Barcelona lifanyike badala yake tarehe 7 Disemba . Tayari shirikisho hilo la mpira wa miguu limeomba kubadilisha gemu hiyo ifanyike Madrid kutokana na hofu ya ghasia za kiraia. (AS)
Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Erling Haaland analengwa na Manchester City. Kijana huyo Mnorway mwenye umri wa miaka 19 ni mtoto wa kiungo wa kati wa Manchester City Alf-Inge Haaland. (Sun)
Mchezaji wa safu ya mashambulizi ya klabu ya Lyon Moussa Dembele anataka kurejea katika soka ya England , huku akiripotiwa kusakwa na Everton na Manchester United. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23- aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Ufaransa ya walio chini ya umri wa miaka -21 awali alichezea klabu ya Fulham. (Football Insider)
Moussa Dembele anataka kurejea katika soka ya England
Manchester United walimtaka na kumfuatilia mchezaji wa Juventus raia wa poland na mlindalango wa zamani wa Arsenal goalkeeper Wojciech Szczesny,mwenye umri wa miaka 29, wakati wa msimu ujao wa soka kabla David de Gea kusaini mkataba mpya katika Old Trafford mwezi uliopita. (Goal)
Wolves wameweka dau kwa ajili ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie mwenye umri wa miaka 22 kutoka AC Milan mwezi Januari . (La Gazzetta dello Sport via Calciomercato)
Wolves wameweka dau kwa ajili ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie
Tottenham na Manchester United ni miongoni mwa klabu kadhaa zilizowasiliana na Borussia Monchengladbach kuhusiana na namna wanavyoweza kumpata Mswiss anayecheza safu ya kati Denis Zakaria ambaye sasa ana umri wa miaka 22. (Bild - in German)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, "si mzuri vya kutosha " kwa Bayern Munich, anasema mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Lothar Matthaus. (Sport 1, via Standard)
Tottenham watalenga kumnunua mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Real Madrid Muhispania Isco,mwenye umri wa miaka 27, kama wataamua kumuuza Eriksen ifikapo mwezi Januari (El Desmarque - in Spanish)
0 COMMENTS:
Post a Comment