HEMED Morroco, Kocha Mkuu wa Mbao amesema kuwa hesabu zake kubwa kwa sasa ni kupata pointi tatu muhimu mbele ya Yanga kwenye mchezo wao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa kesho uwanja wa CCM Kirumba.
Mbao itaingia uwanjani ikiwa na kumbuku ya kulazimisha sare mbele ya Ruvu Shooting kwa kufungana bao 1-1 huku Yanga wakiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 mbele ya Coastal Union.
Akizungumza na Salehe Jembe, Morroco alisema kuwa hawajawa na mwanzo mzuri kutokana na kutengeneza kikosi ambacho tayari amekipata hivyo atapambana kupata ushindi mbele ya Yanga.
“Kwa sasa tuna muda wa kupumzika baada ya kumaliza mchezo na Ruvu Shooting tumesoma makosa yetu na tunayafanyia kazi kwa umakini ili kupata ushindi.
“Tutakuwa nyumbani kufanya kazi kwa ajili ya yale ambayo tumeyafanya msimu huu, nimewaambia wachezaji namna ya kufanya na ni matumaini yetu tutafanya poa, mashabiki watupe sapoti,” alisema Morroco.
Mbao imecheza jumla ya mechi sita imeshinda mechi moja huku ikipoteza mechi moja na kupata sare nne mejikusanyia jumla ya pointi saba.







wafungeni hao eti watasonga mbele.hawajacheza mechi yeyote ya kirafiki..huku tangu wacheze mechi iliyopita ya ligi ambaapo walizawadiwa
ReplyDeletegoli la dhuruma..
Waacha kuwashwa pili pili usiyoila
Deletena kweli wafungeni hao maana si vibonde wenu wakija huko mwanza pigaa aoo churaa fc
ReplyDelete