October 3, 2019


Kiungo mkabaji kipenzi cha Simba, Jonas Mkude huenda akakutana na adhabu ya kukatwa mshahara pamoja na bonasi zake.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu ajiondoe kwenye msafara wa timu hiyo uliosafiri kwenda mikoa ya Mara na Kagera.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kiungo bado anajadiliwa kwenye Kamati ya Utendaji ya timu hiyo baada ya kuchelewa kwenye msafara wa timu bila ya kutoa taarifa.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kati ya adhabu atakayokutana nayo kiungo huyo ni ya kukatwa mshahara na bonasi zake alizotakiwa kupewa.

Aliongeza kuwa katika kikao hicho cha kamati ya utendaji atashirikishwa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya kwa ajili ya kufikia hatma ya sakata hilo la kiungo huyo.

Alipotafutwa Meneja Mkuu wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Hilo suala la Mkude lipo kwa viongozi wa juu ambalo wenyewe ndiyo watalichukulia hatua siyo sisi benchi la ufundi. Jana hakutokea mazoezini tuliyofanya Uwanja wa Gymkhana ambayo na kesho tutaendelea nayo,” alisema Rweyemamu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic