October 3, 2019


Kufuatia kusuasua kwa timu yao, uongozi wa Manchester United umeandaa mipango kabambe ya kusuka upya kikosi chao.

Klabu hiyo ipo taabani kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kwani inakamata nafasi ya 10 ikiwa na pointi tisa tu. Manchester United inasemekana inajipanga kusajili majembe manne ya kuimarisha timu yao.

Klabu hiyo inataka beki mmoja wa pembeni, kiungo, fowadi na straika ili wawe vizuri kwa msimu wa 2020/21. Uongozi wa Manchester United inasemekana ulikutana mwezi uliopita wa Septemba na kuunda kamati ndogo ya kupanga mikakati ya usajili.

Pamoja na kusajili wachezaji wapya lakini pia wanataka kuhakikisha wanambakiza staa wao, Paul Pogba, ambaye inasemekana anataka kuondoka.

Mastaa wanaopigiwa hesabu na Manchester United ni pamoja na kiungo mshambuliaji James Maddison  wa Leicester City, beki Ben Chilwell (Leicester City), winga Jadon Sancho (Borussia Dortmund) na kiungo mkabaji, Declan Rice (West Ham).

Wachezaji hawa pia katika miaka ya karibuni wamekuwa wakichezea timu ya Taifa ya England.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anaamini nyota hao watasaidia kurudisha makali ya miaka ya nyuma ya kikosi hicho. United pia imepanga kuwatema wakongwe Nemanja Matic, Ashley Young na Phil Jones.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic