October 19, 2019


Acheni hofu! Ndivyo Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera alivyowaambia wadau wa klabu hiyo juzi baada ya kurejea nchini. Amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo na kuwaambia amekuja na dawa ya Waarabu.

Yanga itacheza na Pyramids FC ya nchini Misri katika mchezo wa mtoano wa kuwania kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho utakaopigwa Jumapili ijayo katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Zahera mara baada ya kurejea Dar, haraka jana Ijumaa aliungana na timu hiyo kwenye mazoezi ya pamoja yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini.

Zahera alisema kuwa atawavaa Pyramids akiwa tayari anafahamu mbinu na mifumo watakayotumia wapinzani wao, hivyo hana hofu ya pambano hilo. Zahera alisema , amepanga kutumia siku nane katika kuelekea mchezo wake dhidi ya Pyramids kwa ajili ya kuvuruga mipango ya Waarabu ili kuhakikisha anapata ushindi nyumbani na ugenini ambalo ndiyo lengo lake kubwa.

Aliongeza kuwa moja ya mbinu wanayoitumia wapinzani wao ni kucheza soka la pasi katikati huku wakitumia mipira mirefu katika mashambulizi ya kushtukiza.

Kuhakikisha hilo linafanikIwa, Zahera amepanga kuanza kulifanyia kazi katika program yake ya mazoezi ya jana kwa kuwapa majukumu viungo wake Papy Tshishimbi, Feisal Salum na Abdulaziz Makame ili wapinzani wao wasitawale eneo la kiungo.

“Aina ya uchezaji wa soka la Waarabu ninalifahamu vizuri, kwani timu zote za Waarabu wanacheza soka la kufanana la pasi nyingi kwenye safu ya kiungo huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza golini kwa wapinzani.

“Hivyo, tayari nimeshaliona hilo na nimeanza kulifanyia kazi kwenye program yangu ya mazoezi nitakayoanza nayo leo (jana) asubuhi kwa kuwapa mbinu viungo wangu ili wapinzani wasitawale kwenye safu ya kiungo ambayo ndiyo hatari zaidi.

“Nimepanga kutumia dakika za mwanzoni kipindi cha kwanza tutakapokutana kwa ajili ya kuwasoma Pyramids ambazo kwangu zitatosha kupata ushindi wa nyumbani kabla ya kwenda kurudiana kwao, ninafahamu wanakuwa wazuri sana wakiwa kwao lakini nitahakikisha ninakiandaa kikosi vema.

“Na mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC tutakaocheza kabla ya kucheza na Pyramids, nitautumia kama sehemu ya maandaalizi ya kikosi changu kuelekea pambano hilo ,” alisema Zahera ambaye makazi na familia yake ipo Ufaransa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic