October 13, 2019


Straika wa zamani wa Yanga na sasa Kocha Mkuu wa Bandari FC ya Kenya, Benard Mwalala, amesema hawezi kuwa sehemu ya benchi la ufundi kwa mabingwa hao wa kihistoria.

Mwalala aliwahi kutamba na Yanga kwa kufanya vema zaidi miaka ya nyuma lakini baadaye aliondoka na kurejea kwao Kenya.

Akizungumza mara baada ya mcheoz wa kirafiki jana dhidi ya Simba ambao walifungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mwalala alisema ndoto zake ni kwenda mbele zaidi.

Alieleza: "Ndoto zangu kwa sasa ni kujitengenezea mazingira ili niweze kuwa kocha kujiendeleza zaidi kuboresha ndani ya Bandari.

"Siwezi kurejea Yanga kwa sababu Bandari bado wananihitaji."

Baada ya mechi ya jana, Bandari watakuwa na mechi nyingie ya kirafiki kesho ambayo itakuwa dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic