October 13, 2019


Kikosi cha Yanga kesho kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Mechi hiyo itakuwa sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids FC ya Misri Oktoba 27.

Yanga itacheza na Rangers kabla ya kuelekea Mwanza ambapo itaweka kambi maalum kuendelea na maandalizi pamoja na kucheza na timu hiyo ya Misri jijini humo.

Katika mechi hiyo ya kesho, Yanga itamkosa Kocha wake Mkuu, Mkongomani, Mwinyi Zahera ambaye amejiunga na kamb ya timu ya taifa ya Congo kwa majukumu ya Ukocha Msaizidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic