October 19, 2019


KIUNGO wa PSG, Neymar Jr amesema kuumia kwake ni pigo kubwa kwa kuwa alitaka kuisaidia timu yake.

Neymar Jr aliumia akiwa na timu yake ya Taifa ya Brazil wakati ikimenyana na Nigeria kwenye mchezo wa kirafiki.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa pamoja na kwamba hakai nje muda mrefu lakini anaamini hata akikosa mechi moja ni pigo kubwa.


"Inauma kuona namna gani naweza kuumia kwa kukosa kucheza kutokana na kuwa na majeraha, ninaamini nitakuwa nje Kwa muda mchache. 

"Sipendi hali hii itokee kwa kuwa PSG inanihitaji nami naihitaji naumia sana kukaa nje, japo naamini itakuwa kwa muda mchache kwangu ni pigo" amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic