October 29, 2019


Imeelezwa kuwa Kocha Kim Poulsen, amesema yupo tayari kurejea tena nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi na Yanga.

kauli hiyo imekuja kutokana na kupokea maswali mbalimbali juu ya tetesi zilizoonekana jana kuwa anahitajika Yanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera pale Yanga.

"Kwa sasa nipo Denmark naendelea na project mbalimbali za FIFA.

"Sina mkataba na timu yoyote kwa leo nimepokea simu nyingi sana kutoka Tanzania zikiniuliza kujiunga na klabu ya Yanga.

"Yanga ni timu kubwa sana Tanzania naamini itanipa fursa ya kusaidia maendeleo ya soka la Afrika kama nitaenda kufanya kazi nao, mimi nipo tayari kurudi Tanzania."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic