ETIENNE Ndayiragije amepewa kandarasi ya mwaka mmoja kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania ambayo imefuzu kucheza fainali za Chan 2020 nchini Cameroon.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeeleza kuwa sababu kubwa iliyofanya Ndayiragije aweze kupewa dili hilo ni kukidhi vigezo vilivyowekwa.
Kabla ya uteuzi huo ambao umetangazwa rasmi leo Ndayiragije alikuwa kaimu kocha alichukua mikoba ya Emanuel Ammunike raia wa Nigeria.
Kamati ya Utendaji imeamua kumpa dili hilo baada ya mapendekezo ya Kamati ya Ufundi ya TFF ambayo ilipitia maombi ya makocha mbalimbali walioomba nafasi hiyo.
Pia Ndayiragije aliweza kuiongoza Stars kuingia hatua ya makundi ya mechi za kombe la Dunia kwa kuifunga Burundi.
0 COMMENTS:
Post a Comment