Bao hilo pekee limepatikana mnamo dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza kwa Otieno Onyango kujifunga.
Ushindi huo unaipa rasmi Tanzania kikombe hicho ambacho mashindano yake yalikuwa yanafanyika nchini Uganda.
Baada ya ushindi huo, Ngorongoro watarajia kurejea nchini kuanzia kesho.
Baada ya ushindi huo, Ngorongoro watarajia kurejea nchini kuanzia kesho.
Hawa vijana wa Ngorongoro ndio wa kuanzia ukarasa mpya katika soka letu Tanzania kwa ngazi ya taifa . Kwanza kabisa hawa vijana wapatiwe elimu maalum ya psychology kuhahakisha hawavimbi vichwa na kujiona wamefika. Pili kuwe na jitihada za makusudi kuhakikisha hawa vijana wanakuzwa pamoja. Tatu wapatiwe mafunzo ya uzalendo zaidi.Serikali muda umefika kuekeza kwa vijana wenye vipaji na hapana shaka hawa vijana wa Ngorongoro wana vipaji na vinatakiwa kukuzwa. Wapatiwe mechi nyingi za majaribio na nchi zilizobobea zaidi kisoka. Hapa kwa Ngorongoro ndipo tunaweza kujenga utambisho wa soka la Tanzania kama tukiamua. Mpira sasa sio wa vipaji peke yakei bali ni wa kuvijenga vipaji na kutengeneza watu wa kazi. Kwa hivyo wakati ni huu kwa wadau wa soka na maendeleo ya Tanzania kuhakikisha tunajenga timu ya Taifa imara kwani Tanzania kimichezo duniani ni sawa na Taifa lililokufa au Taifa lenye watu wasio na nguvu za ushindani miongoni mwa wanadamu wa kawaida hivyo wakati wa kupambana na kuondoka na hali hiyo ni huu kwani nguvu tunayo,uwezo tunao ila tunatakiwa kubadilika katika mifumo yetu ya kiakili nakuwa watu wenye uthubutu wa kuweza kufanya mambo makubwa zaidi kuliko hali ya sasa ambayo viongozi wetu hasa wa sekta ya michezo kuonekana kukubali kwamba ya sisi watanzania ni wamiliki halisi wa viwango duni vya michezo duniani na ni kama vile tunachekelea kubakia huko miaka nenda miaka rudi hakika Mungu siku moja akisikie kilio chetu wapenda michezo Tanzania ili atuletee Magufuli katika sekta ya michezo na ndani ya mwaka mmoja tuone mabadiliko ya kweli Amin.
ReplyDelete