October 5, 2019


JAMES Milner, kiungo mshambuliaji wa Liverpool leo ameiokoa timu yake kuambulia pointi moja mbele ya Leicester City uliopigwa uwanja wa Anfield.

Sadio Mane alianza kuandika bao la kwanza kwa Liverpool dakika ya 40 lilidumu mpaka dakika ya 80 ambapo Leicester City walisawazisha kutokana na uzembe wa mabeki wa Liverpool dakika ya 80.

Mshambuliaji wa Liverpool Mohammed Salah aliumia na kufanyiwa mabadiliko dakika ya 88 nafasi yake ilichukuliwa na Lalana.

Dakika ya 90 Mane alichezewa rafu na mabeki wa Leicester City na mwamuzi akaamua ipigwe penalti na walijiridhisha kwa kuangalia VAR.

James Milner alimaliza utata kwa kuachia mshuti mkali uliozama wavuni mazima.

Liverpool inazidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza michezo nane bila kupoteza na Leicester City inakuwa nafasi ya tatu ina pointi 14.

2 COMMENTS:

  1. We mwandishi kweli mtihani ni ushauri wa bure kabla ya kupublishi habari zako zipitie na uzisome kwanza ni aibu kubwa kila kukicha unarudia makosa yale yale kichwa cha habari zako hazilingani na habari unayo andika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic