AARON Connolly wa Brighton alikuwa ni mwiba leo mbele ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Ligi Kuu England kwa kuwatandika mabao mawili wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Bao la Kwanza lilipachikwa na Neal Maupay dakika ya tatu na iliwabidi wasubiri mpaka dakika ya 32 kuandika bao la pili wakiwa nyumbani.
Mabao mawili ya ushindi yalifungwa dakika ya 32 na 65 yaliipoteza kabisa Tottenham kwenye reli na mfumania nyavu alikuwa ni Connoly.
Matokeo hayo yanaifanya Tottenham kuwa nafasi ya sita wakiwa na pointi 11 na wamecheza michezo nane.
Brighton inakuwa nafasi ya 13 ikiwa imecheza Michezo nane na imekusanya pointi tisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment