WAZUNGU WALETA KUFURU YA UWANJA YANGA
Mmoja wa viongozi wa Yanga aliidokeza Spoti Xtra kwamba Septemba 23 walipokea barua kutoka kwa kampuni ya Patel Engeneering ikiomba kuingia makubaliano na Yanga juu ya ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa mazoezi na mechi pale Jangwani.
Mbali na hivyo kiongozi huyo anasema kwamba ujenzi huo wa kisasa utahusisha hosteli na hoteli inayoweza kulaza mamia ya watu tena pamoja na maduka ya maana.
Kubwa kuliko ni kwamba Spoti limedokezwa kwamba Patel Engeneering wanataka Uwanja huo wa Jangwani uingize mashabiki 65,000 ikiwa ni 5000 zaidi ya Uwanja wa Taifa ambao ndio mkubwa na wa kisasa zaidi nchini.
“Hiyo kampuni ya ujenzi wanasema imesajiliwa Uingereza na inaonyesha ipo kwenye nchi nyingi za Ulaya mpaka Afrika ipo Msumbiji na Eritrea,”kilisema chanzo chetu ndani ya uongozi huku akionyesha kwa mbali nakala ya barua waliyotumiwa huku akigoma kuisoma ndani kwa madai ni siri kubwa ya sekretarieti mpaka wakapokubaliana.
“Wao wanaomba kazi ya kufanya ujenzi wa kisasa pale Jangwani, watajenga Uwanja mkubwa zaidi ya Taifa, Hoteli ya maana lakini yote hayo yatakuwa kwenye makubaliano maalum ya miaka zaidi ya 20.
Wao wataendesha Uwanja na kila kitu kibiashara kwa makubaliano maalum mpaka fedha irudi. “Wao watasimamia kila kitu,lakini na klabu itanufaika kimapato pia.
Sisi tukishakubaliana nao na kuwapa kazi ndio watakuja Tanzania kuweka sawa hayo mambo mengine ya kimkataba na kampuni yao kila kitu kitakuwa hapa,”alisema kiongozi huyo.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa Wazungu hao wamewapa masharti kwamba kama wameipenda ofa hiyo ya ujenzi mpaka Novemba 30 wawe wamethibitisha kwa maandishi vinginevyo itakuwa imemalizika muda wake.
Hakuna kiongozi yoyote wa juu wa Yanga aliyekuwa tayari kufafanua kwa kina ishu hiyo jana, lakini Spoti Xtra limejiridhisha kwamba bado wanatafakari kwavile ni kitu kipya na kinachohitaji umakini kwavile ni ya miaka mingi.
Kama dili hiyo ya Yanga ikikamilika inamaanisha kwamba klabu hiyo itaingia kwenye historia ya kuwa klabu ya kwanza kumiliki uwanja, hosteli na hoteli za kisasa zaidi Barani Afrika.
CHANZO: SPOTI XTRA
Porojo tu hizo. Mlishatuonesha michoro ya uwanja siku nyingi, hata hatujui iliishia wapi.
ReplyDeleteHuwa hamjielewei viongozi mpo kwa ajili ya kupiga dili tu
ReplyDeleteacheni utoto kujaza watu 20,000 tatizo kisha ujengwe wa 65,000 wahuni wakubwa nyinyi kawadanganyeni mademu zenu tena sio wake
ReplyDeleteKusema ukweli viingilio ni vya juu sana angalau wangefanya kima cha chini 5,000 cha juu 50,000 lengo lisiwe mapato bali liwe ni kuujaza uwanja sasa sidhani kama kwa viingilio hivyo mtaujaza uwanja KWANI HII MECHI NI YA MUHIMU SANA KWA MAANA NYINGINE NAFASI NI MOJA TU KUSHINDA MECHI HII YA NYUMBANI HAKUNA NAFASI NYINGINE MSIFIKIRIE KWENDA MISRI KUSHINDA....USHINDI WENU NI KUUTUMIA UWANJA NA KUHAMASISHA MCHEZAJI NO. 12 AINGIE KUTOA HAMASA NA USHANGILIAJI. Halafu suala la vibali vya CAF watu wanachanganywa mlisema mmepokea barua ikiwaruhusu kuwatumia leo mnasema kanuni...sasa kwanini mliwapa matumaini watu kuwa watatumika halafu leo mmeyazima matumaini hayo?
ReplyDeletePorojo tu hamna kitu....gazeti ili liuzwe
ReplyDelete