WACHEZAJI
wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wamesema kuwa wapo tayari kwa mchezo
wa marudiano wa kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Chan dhidi ya Sudan
utakaochezwa leo.
Stars
inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza Kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja
wa Taifa Kwenye michuano hii inayohusisha wachezaji wa ndani.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na Saleh Jembe, wachezaji hao wamesema kuwa wanatambua
ushindani ni mkubwa ila wapo tayari kupambana kupata ushindi utakaowapa nafasi
ya kusonga mbele.
Metacha
Mnata, mlinda mlango wa Stars amesema:-" Tunamshukuru Mungu morali ipo
sawa kwa wachezaji na tumejiandaa kiasi cha kutosha kupeperusha vema bendera
yetu, tunaimani ya kupata matokeo mazuri kwani hilo ndilo ombi letu, tutapambana.
Jonas
Mkude, Kiungo wa Stars amesema:- "Kila kitu kipo sawa tunamshukuru Mungu,
kilichobaki ni kupambana kutafuta matokeo kwani maandalizi yetu yapo vizuri, kikubwa
dua kwa mashabiki nasi tutafanya vizuri.
Idd
Seleman 'Nado' mshambuliaji wa Stars amesema :-" Tunajua haitakuwa kazi
rahisi kwani wapinzani wetu sio wa kuwabeza wanatutambua ukizingatia tulicheza
nao, hilo halitupi taabu tumejipanga kufanya kweli mashabiki watuombee nasi
tutapambana uwanjani," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment