Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera, umesema kuwa hauna hofu kabisa na Pyramids FC ambayo watakutana nayo katika mechi ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga itakuwa na mechi dhidi ya waarabu hao kutoka Misri ambapo mechi itachezwa jijini Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Oktoba 23 mwaka huu.
Zahera ambaye alikuwa na timu ya taifa ya Congo, amesema hahofii gharama za wachezaji wa Pyramids huku akisema anachokifanya ni kuwaandaa wachezaji wake.
Ameeleza kuwa gharama hazizungumzi bali namna timu ilivyojiandaa inaweza kuamua matokeo ya mechi hiyo.
"Sisi tunazidi kujiandaa vizuri kuelekea mechi na Pyramids, hatuna hofu na gharama za wachezaji wao, tunajipanga kuhakikisha tunaondoka na matokeo kwa sababu tutakuwa tunatumia uwanja wetu wa nyumbani."
0 COMMENTS:
Post a Comment