October 18, 2019


Klabu ya Yanga imekuwa ya kwanza kuwakaribisha AS Roma ya Italy katika ulimwengu wa Kiswahili kwa klabu za nyumbani baada ya kufungua ukurasa wao rasmi utakaokuwa unapasha habari kwa lugha pendwa na mama hapa nchini huko Twitter.

Ukurasa huu umekuja mara baada ya siku kadhaa nyuma bosi wa klabu hiyo kusema watauanzisha na rasmi umefunguliwa jana na kuanza kupasha habari mbalimbali za klabu hiyo.

Yanga nao kupitia ukurasa wao wa Twitter waliwakaribisha Roma kwa kukomenti baada ya tu ya Roma kuutambulisha rasmi kama inavyoonekana hapo chini.

Kufunguliwa kwa ukurasa huo inaonesha namna gani lugha ya Kiswahili inazidi kukua zaidi duniani.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic