October 3, 2019


Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesisitiza kuwa staa mpya wa kikosi hicho, Eden Hazard atakuwa bora kwani hata yeye alianza kwa kusuasua alipojiunga na timu hiyo mwaka 2001.

Madrid imemsajili Hazard msimu huu akitokea kwenye kikosi cha mabingwa wa Ligi ya Europa, Chelsea ambayo inashiriki Ligi Kuu England.

Alisajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 88.5 msimu huu, ambapo alipata majeraha ambayo yalimuweka nje na alikuja kuanza kucheza dhidi ya Paris Saint Germain kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kupoteza kwa mabao 3-0.

Hazard pia alishindwa kutamba mbele ya Sevilla na Atletico Madrid, lakini kocha wake Zidane amesema ni muda tu ila atakuwa bora tu.

“Siwezi kumwambia ni namna gani anatakiwa kucheza,”alisema kocha huyo wakati wakijiandaa na mchezo wao na Club Brugge kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa jana na kuongeza.

“Anajua ni kitu gani zaidi tunahitaji kutoka kwake na tunafahamu yeye ni mchezaji wa aina gani, hivyo sina wasiwasi kabisa.

Najua atafanya vizuri hivyo tusiwe na hofu na wachezaji wapya. “Kinachomtokea Hazard kwa sasa kiliwahi kunitokea ndiyo maana sina hofu najua atakuwa sawa ni muda tu. Ilikuwa mbaya kwangu nilipotua hapa nikitoka Italia ilinichukua kama miezi mitatu kuwa sawa.

“Ndiyo kinachotokea kwa Hazard, najua ataenda kufanikiwa akitulia na hana tataizo lolote kwa sasa atafanya vizuri yeye pamoja na timu kwa ujumla.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic