November 17, 2019


Achana na haabari za kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya KMC jana katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Azam Complex, uaambiwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba SC wameingiwa na hofu juu ya kuumia kwa beki Erasto Nyoni.

Nyoni ambaye amekuwa bora kwa muda wote tangu asajiliwe Simba aliumia juzi wakati akiitumikia timu ya taifa 'Taifa Stars' katika mechi dhidi ya Equatorial Guinea ambayo ilichapwa mabao 2-1 jijini Dar es Salaam.

Nyoni aliumia goti katika mechi hiyo ambayo ilikuwa ni ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Kuumia kwa Nyoni kunaleta hofu kwa mashabiki na wanachama wa Simba kutokana na ubora wake ndani ya dimba.

Taarifa za ndani zinasema Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ni kama ameingia na hofu pia juu ya kuumia kwa Nyoni ambaye amekuwa akianza katika mechi nyingi.

Nyoni hajajumuishwa katika kikosi cha Stars ambacho kimesafiri jana kuelekea Libya kwa ajili ya mchezo mwingine wa kuwania fainali hizo utakaopigwa Novemba 19.

6 COMMENTS:

  1. kwa hiyo simba ya sasa ni ya nyoni, maana mmeacha kuelezea mchezo mnasema majeraha ya nyoni, kufungwa ni kufungwa, kwan nyoni ni beki pekee pale simba/

    ReplyDelete
    Replies
    1. soma vizuri ww hapo wazungumzii kukosekana kwa nyoni wanasema kuumia kwa nyoni ni pigo kwa simba kilaza ww

      Delete
  2. Kocha anaingiwa hofu ilihali yeye ndio anawaharibu akina Mlipili

    ReplyDelete
  3. Na siku akiumia kagere mikia wanashuka daraja

    ReplyDelete
  4. Ko ni pigo kwa simba tu,, na kwa stars vp? Pale alipotaka kutandika daruga mkuu was mkoa was Dar , alizungumzia asisitafu kuchezea simba au stars?

    ReplyDelete
  5. Aisee nyoni namkubali sana,kikubwa apatiwe matibabu sahihi na kwa wakati sahihi,get well soon nyoni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic