November 17, 2019



Baada ya komediani maarufu wa kike Bongo, Annastazia Exavery ‘Ebitoke’ kukinukisha kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa mwigizaji Yusuf Mlela, jamaa huyo amejiongezea ulinzi.

Jumatatu wiki hii, Ebitoke alivamia mkutano huo kwenye Hoteli ya Protea jijini Dar na kumfanyia vurugu mpenzi mpya wa Mlela aliyetajwa kwa jina moja la Stella au Beyonce.

Ebitoke alisema alifanya hivyo kwa madai kuwa Beyonce ndiye aliyesababisha jamaa huyo kumtema.

Kufuatia ishu hiyo, Mlela ameona kuna kila sababu ya kuongeza mlinzi binafsi (bodigadi) ili kumkabili Ebitoke atakapokuwa akimfuatilia.

Alipoulizwa na Gazeti la Ijumaa juu ya kuongeza bodigadi wa pili ili kumkabili Ebitoke, Mlela alikiri kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Ebitoke naye ametangaza vita na Mlela akisema kuwa, kila sehemu ambayo jamaa huyo atatia mguu, lazima aliamshe dude hadi pale atakapokubali kumlipa gharama zake zote walizokuwa wanakula bata pamoja wakati wa penzi lao huku akimdanganya atamuoa.

Juzi, Ebitoke aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika; “Nasikia kuna mtu anataka kunipiga!”

Posti hiyo ya Ebitoke ilitafsiriwa kuwa, yupo tayari kwa mapambano muda wowote ule kwa mpenzi wa sasa wa Mlela aliyempa kichapo hadi kuvuliwa wigi na kumwacha na kipilipili kichwani.

Wakati akipokea kichapo hicho, Beyonce alisikika akisema kuwa Ebitoke ni mtu mdogo kwake na atamuonesha yeye ni nani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic