TIMU ya
Alliance FC imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu za
moja kwa moja mbili ndani ya msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa
na Vodacom (VPL) mwaka 2019/20 kwenye mchezo mmoja.
Kwenye mchezo
uliochezwa Juzi dhidi ya Mbeya City uwanja wa Nyamagana nahodha wa Alliance FC
Israel Patrick alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 52 kwa kosa
la kumdhalilisha mchezaji wa Mbeya City licha ya mwamuzi kupuliza kipyenga.
Pia dakika
ya 71 John Mwanda mlinda mlango wa
Alliance alionyeshwa kadi nyekundu ya
moja kwa moja kwa kosa la kumchezea rafu isiyo ya lazima mchezaji wa Mbeya City
mara mbili licha ya filimbi kupulizwa.
Iliwalazimu
Alliance kumbadilisha mchezaji Siraj Juma ambaye ni mchezaji wa ndani kuvaa
gloves za Mwanda kutokana na timu yake kumaliza idadi ya wachezaji wa
mabadiliko ndani ya uwanja ambao ni watatu.
Licha ya
Alliance kucheza pungufu kwa muda wa dakika 19 kwenye uwanja wa Nyamagana, Mbeya City ilishindwa kutikisa
nyavu za Juma ambaye alipangua mashuti matatu akiwa langoni na kufanya mchezo
kukamilika kwa sare ya 0-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment