LIONEL Messi mshambuliaji wa Barcelona amempiga bao mpinzani wake Cristiano Ronaldo kwa kutupia mabao mengi ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Barcelona ipo kundi F imejihakikishia nafasi ya kufuzu michuano hiyo mikubwa baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 wakati wakimenyana na Borussia Dortmund.
Bao lake moja alilofunga huku mengine mawili yakifungwa na Luis Suarez pamoja na Antoine Griezmann yameibeba Barcelona.
Sasa Messi anafikisha jumla ya mabao 34 akiwa ni kinara kwa wachezaji waliofunga mabao mengi ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Cr 7 akiwa amefunga jumla ya mabao 33 akiwa nafasi ya pili.
Cr7 akifunga uje kutuletea mrejesho haraka sana.
ReplyDelete