November 18, 2019


Baada ya kujihakikishia nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba, mshambuliaji, Miraji Athuman ‘Sheva’ anataka nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Miraji ameibukia kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Simba, hasa katika kipindi hiki ambacho nahodha wa timu, John Bocco akiwa nje ya uwanja akiuguza majeraha, ambapo katika michezo nane aliyocheza amefunga mabao manne na kutoa pasi tatu.

“Siku zote nimekuwa nikiomba niwe moja ya wachezaji bora wa Tanzania katika kizazi hiki.

"Hivyo kwa nafasi ambayo nimeipata sasa katika klabu yangu na Taifa nitaitumia vizuri ili niendelee kudumu na kuaminiwa zaidi,” alisema Sheva ambaye ni miongoni mwa matunda ya timu ya vijana ya Simba enzi za Seleman Matola.

3 COMMENTS:

  1. Penye nia basi kuna njia na kama kweli Miraji una mikakati ya dhati yakuwa mchezaji wa kutumainiwa Taifa stars basi hizi mechi za kufuzu Afcon ukizitendea haki si kwamba utakuwa mchezaji wa kutumainiwa Taifa stars tu bali zitakutowa kabla ya wakati kufika. Hapo mlipo hivi sasa kwenye ardhi ya Tunisia si pakwenda kufanya kazi ya mazoea kama bongo. Hapo hapo ukijotoa kuliko kawaida hurudi Bongo na hili si kwa Miraji bali kwa wachezaji wote wa Taifa stars huu ni wakati wa kujitangaza kwa vitendo. Hizi ni mechi za kimkakati kwa kila mchezaji wa Taifa stars kwa hivyo piganeni kana kwamba kila mechi ni fainali hasa ugenini kwani ukionesha ujasiri ugenini ni kigezo tosha kuwa unajiamini na ukiweza kujiamini ugenini ni kujijimengea mazingira ya kufanya kazi sehemu yeyote ile na ni kujipanulia wigo mpana wa kupata ajira. Wachina wanaamini no risk no reward,yaani bila ya kujitoa muhanga ni vigumu kukipata kile unachokitaka kwa ukamilifu.

    ReplyDelete
  2. Naamini kijana huyu atafikia malengo. Nimemfuatilia muda mrefu. Ni mpambanaji.Makocha wampe nafasi zaidi. All the best!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic