UONGOZI wa Singida
United umesema kuwa kwa sasa upo tayari kurejea kwenye mapambano baada ya kuwa
chimbo kwa muda wa wiki moja kutokana na ligi kusimama.
Singida United iliyo
chini ya kocha mkuu Ramadhan Nswazurimo imeanza kwa mwendo wa kusuasua msimu
huu ikiwa haijaambulia ushindi hata mechi moja kati ya 11 ambazo imecheza mpaka
sasa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa
wamekuwa na mwendo mbovu jambo lililowafanya watulie kutafuta dawa ya matatizo
yao.
“Ukweli unaonekana
kwani hatujawa na mwenendo mzuri kwenye ligi mpaka sasa tunawaomba mashabiki
wasahau ya nyuma kwa sasa tunaanza upya kufanya kweli.
“Tuna mechi mbili
nyanda za juu kusini tutapambana kupata pointi sita ambazo zitaturejesha kwenye
ushindani ambao tunauhitaji, tutaanza na Mbeya City Jumamosi kisha Tanzania
Prisons Novemba 25,” amesema Catemana.
Singida United ipo nafasi ya 20
imejikusanyia pointi nne imelazimisha sare nne na kupoteza jumla ya mechi saba
na imefungwa mabao 15.
0 COMMENTS:
Post a Comment