ARSTICA
Cioba, Kocha Mkuu wa Azam FC raia wa Romania ameonja chungu na tamu ya Ligi Kuu
Bara msimu wa 2019/20 kwa kupata ladha ya matokeo yote matatu ya mpira ndani ya
dakika 270 kwenye mechi tatu ambazo amekaa benchi kwa kufungwa kupata sare na
kushinda.
Cioaba
amepewa kandarasi ya mwaka mmoja kuinoa Azam FC iliyokuwa chini ya Etienne
Ndayiragije ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa
Stars alianza kupokea kichapo cha bao 1-0 uwanja wa Mabatini alipocheza na Ruvu
Shooting ya Masau Bwire.
Kabla
hajakaa sawa alibanwa mbavu na Kagera Sugar ya Mecky Maxime kwenye mchezo
uliochezwa uwanja wa Azam Complex kwa kupata sare ya bila kufungana kabla ya
kuonja ladha ya ushindi mbele ya Biashara United kwa ushindi wa mabao 2-1
uwanja wa Azam Complex.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema
kuwa kikubwa ambacho wanakihitaji kwa sasa ni ushindi kutokana na kuwa na
kikosi imara ambacho kinaushindani mkubwa.
“Tuna kikosi
kipana na chenye wachezaji wenye uzoefu kikubwa ambacho tunakihitaji ni ushindi
kwa mechi zetu zilizobaki na hatupaswi kuwa na kiburi kwa ushindi ambao
tumepata hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kazi bado inaendelea,”
amesema Popat.
Ushindi huo
unaifanya Azam FC ifikishe jumla ya 13 baada ya kucheza mechi 7 ikiwa imeshinda
nne imetoa sare moja na kupoteza mechi mbili ndani ya ligi kuu msimu huu ipo nafasi ya 11.
0 COMMENTS:
Post a Comment