JUMA Mgunda,
Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa kuna baadhi ya mechi wachezaji wake
wamekuwa wakicheza chini ya kiwango jambo ambalo linawaweka kwenye nafasi mbovu
kwenye ushindani wa ligi.
Coastal
Union ya Tanga imecheza jumla ya mechi 10 ikiwa imeshinda mechi tatu pekee na
kutoa sare mechi mbili huku ikiambulia vichapo mechi tano msimu huu zinazoipa
pointi 11 nafasi ya 13 kwenye msimamo.
Mgunda amesema kuwa ana kila sababu za kuwapongeza wachezaji wake
kwa namna wanavyopambana uwanjani ila kuna wakati huwa hawachezi vile
anavyotarajia jambo ambalo linawatoa kwenye reli ya ushindani.
“Kuna mechi
nyingi ambazo tumecheza na kupoteza ukitazama namna ambavyo wachezaji
wanacheza unapata picha kwamba hawajacheza kwenye kiwango chao cha siku zote
jambo ambalo linatufanya tunakosa matokeo.
“Ila
kushindwa mara moja haina maana kwamba ndio mwisho wa mapambano hapana
tunajipanga na kufanyia kazi makosa yetu nina amini tutakuwa sawa kwani makosa
ni sehemu ya mchezo kikubwa ni kuyapunguza ili yasitokee kwa kuongeza umakini,”
amesema.
Soka la bongo halina tofauti na soko la bangi
ReplyDelete