November 10, 2019


PEP Guardiola Kocha Mkuu wa Manchester City ameshindwa kuivunja rekodi iliyodumu kwa muda wa siku 900 kwenye uwanja wa Anfield kwa timu ya Liverpool kushindwa kupoteza mchezo wake wa Ligi Kuu England pamoja na na mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Ushindi wa mabao 3-1 waliyopata leo uwanja wa Anfield yameongeza mlima kwa City kupindua meza kwa Liverpool ambayo imezidi kujikita kileleni. 

Fabinho alianza kuitungua City dakika ya 7 kwa mshuti mkali akiwa nje ya 18 kabla ya Salah kuandika bao matata kwa kichwa akiwa ndani ya 18 dakika ya 13.

Mpaka muda wa mapumziko City ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 jambo lililozidisha uzito kwa City kwenda kujadili namna ya kupindua meza kibabe.

Sadio Mane, mshikaji wake Guardiola ambaye anadai Mane ni bingwa kujiangusha alifunga bao la 3 kipindi cha pili dakika ya 51 na kufanya Liverpool izidi kujiweka salama ndani ya Anfield.

Bernardo Silva mnyama hakuwaacha salama Liverpool kwa kuwatungua mbao wa kufutia machozi dakika ya 78 na kufanya ngoma iwe 3-1.

Mambo yalipozidi unga Klopp aliamua kumtoa nje Salah nafasi yake ikachukuliwa na beki Joe Gomez ambaye alizinguana na Sterling dakika ya 89 na ugomvi wao uliamuliwa na beki kitasa Dijk.

Guardiola kwenye benchi hakuwa na utulivu kwani likuwa akimlaumu mwamuzi wa kati kwamba hana maamuzi sahihi kwa kuonyesha vidole viwili akidai ni penalti ambazo wamenyimwa kihalali kabisa.  

Christian Bentenke alikuwa mwanaume wa mwisho kuwanyamazisha mashabiki wa Anfield kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ilikuwa Aprili 2017 akiwa na Crystal Palace.


Ushindi wa leo unaifanya Liverpool kuwa nafasi ya kwanza ikiwa na pointi zake 34 huku ikiwaacha City nafasi ya 5 na pointi zao 25 na kuwaacha kwa jumla ya pointi tisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic