November 10, 2019


ANDREAS Pereira nyota wa Manchester United leo ameuwasha moto kwenye mchezo wao wa 13 mbele ya Brighton wakiwa uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford.

Davy Propper alijifunga dakika ya 19 na kuipa United bao la pili huku lile la kufutia machozi likifungwa na Lewis Dunk dakika ya 64 kwa Brighton kabla ya msumari wa tatu kupachikwa na Marcus Rashford dakika ya 66 na kuifanya United kushinda kwa mabao 3-1.

Vijana wa Kocha Mkuu Ole Gunnar Solskjaer Leo wamechangamka na kuanza kurejea kwenye ubora wao taratibu baada ya kupoteza mchezo wake wa Ligi mbele ya Bournemouth kwa kufungwa bao 1-0 ilishinda mabao 3-0 Ijumaa mbele ya Partizan mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ushindi huo unaifanya United kufikisha jumla ya pointi 16 ikiwa imeshinda mechi yake ya nne leo na imepoteza nne na Sare nne pia.

Brighton imebakiwa na pointi zake 15 ikiwa nafasi ya 10 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic