November 15, 2019



MIAKA 39 ambayo Taifa letu la Tanzania lilikaa bila kufuzu michuano ya Afcon inapaswa itupe maswali magumu kwamba tuna kazi ya kuendeleza rekodi nzuri ambayo tuliinzisha.

Timu ya Taifa ya Tanzania ilifanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Afcon nchini Misri licha ya kushindwa kufanya vema nchini Misri kwa kupata kichapo mechi zake zote.

Stars ilifanikiwa lengo lake la awali kuvunja mwiko wa miaka 39 ikashindwa kupata matokeo chanya kwani iliambulia mabao mawili pekee kwenye mechi zake nne na ikakosa pointi hata moja.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania mnajukumu lingine mbele yenu kwa sasa ambalo linawahusu wenyewe tena bila kusahau ni kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Mnaingia vitani Ijumaa kupambana na Equatorial Guinea sio kazi nyepesi ambayo ipo mbele yenu kwa sasa hasa ukizingatia kwamba mpira wa sasa ni ushindani na kila timu inatafuta ushindi.

Nina amini kwamba mnatambua nini mnahitaji na mna kazi ya aina gani ambayo ipo mbele yenu kwa sasa hivyo ni muhimu kuungana kwa pamoja kupambana kwa ajli ya Taifa hicho ndicho kinatakiwa.

Kwa hatua ambayo mnaanza nayo mnapaswa mtambue kwamba ni mwanzo ambao utaleta hatua nyingine nzuri ya kufikia mafanikio ambayo ni wimbo wa kila mtanzania na mashabiki.

Mna kazi ngumu ya kuwaaminisha watanzania kwamba hamjaitwa bahati mbaya kwenye kikosi cha timu ya taifa ambacho kinawakilisha bendera ya taifa kiujumla na jukumu ni zito kwa kweli.

Kwa sasa akili zenu zinapaswa ziwe kwenye kufuzu Afcon kwa namna gani kabla hamjaanza kufikiria mambo mengine ambayo mmekuwa mkiyawaza siku zote kabla ya kuitwa timu ya taifa.

Kikubwa kinachohitajika kwenye mpira ni maadalizi mazuri na sahihi hali itakayosaidia kupatikana kwa matokeo chanya uwanjani hakuna uchawi mwingine hapo.

Hivyo wachezaji rekodi ambayo mliivunja mnapaswa mpambane iwe ya muendelezo kwa sasa kutokana na mazingira kuwahukumu endapo mtabweteka.

Pia jambo jingine ambalo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatakiwa lishtuke mapema ni hali halisi iliyopo kwenye mashindano ya kimataifa.

Umuhimu wa michuano hii ni hamasa kwa kuwapa taarifa mashabiki pamoja na wadau waipe sapoti timu yetu ya Tanzania ambayo ina kazi kubwa ya kufanya.

Kila mmoja ahusike kupambana kwa ajili ya mafanikio ya timu ambayo bado haijawa sehemu mbaya kwenye michuano ya kimataifa kwa mechi zake za hivi karibuni.

Matarajio ya mashabiki ni kuona kwamba hesabu zinaanza kuhesabiwa hapa nyumbani kwa kupata ushindi mapema jambo litakaloongeza nguvu ya kujiamini.

Maandalizi ni kitu cha msingi kwa wachezaji kuzingatia maelekezo ambayo wanapewa ili kuyatumia kwenye mechi bila kusahau kwamba wanapaswa waongozwe na nidhamu.

Kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni mipango makini ili kupata matoke mazuri kwenye mchezo wa Ijumaa ambao matarajio ya mashabiki ni kuona kwamba wachezaji wanapata matokeo chanya.

Kila kitu kinawezekana iwapo kila mmoja atashiriki kikamilifu kwenye majukumu yake kwani mchezo wa mpira ni majukumu ndani na nje ya uwanja.

Wachezaji mnapaswa mjitume na kuwa na uchu wa mafanikio kwenye mechi zote ambazo mtacheza kwa sasa uwanja wa taifa.

Imani yangu ni kwamba kwa kuwa mliweza kufuzu hivi karibuni basi ni wakati mwingine wa kupata matokeo chanya kwenye mechi hii ambayo mtakuwa nyumbani.

Mtambue kwamba kwa kila hatua ambayo mnaipiga kwa sasa ni mafanikio kwa Taifa kwani viwango vya soka taratibu vinapanda hali inayopandisha ramani ya soka letu.

Mashabiki wte kwa sasa ni suala la kutambua kwamba ni wakati wa kuipa sapoti timu ya taifa bila kujali itikadi za timu zetu ambazo tunashabikia tukiwa nyumbani.

Muda wa kujiwekea matabaka na makundi usiwepo tuwe 
kitu kimoja kwa kuwa taifa letu ni moja na asili yetu ni moja kuishi kwenye upendo muda wote.

Hakuna haa ya kutengana katika hili kwa kuwa kushindwa kwa mmoja kutimiza wajibu wake kutaleta maumivu hapo baadaye.

Tukiungana tutapata matokeo chanya ambayo ni faida kwetu sote watanzania ambao ni mashabiki na wadau wa timu yetu.
Chuki za mashabiki hazijengi bali zinabomoa na kufanya mpira wetu ubaki palepale ulipo tubadilike na tupeane sapoti mwanzo mwisho kwa maendeleo yetu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic