UONGOZI wa Kagera Sugar
umesema kuwa kwa sasa ni lazima wapambane kuendelea na moto wao ambao wameanza
nao msimu huu kwa kupata matokeo chanya kwenye mechi zao zote watakazocheza.
Mecky Maxime, Kocha
Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wanatambua ushindani uliopo ndani ya ligi
jambo linalowafanya wapambane kuendeleza wimbi la ushindi kwa timu.
“Ligi ni ngumu na kila
timu inahitaji matokeo jambo ambalo linafanya nasi tupambane kupata ushindi
kwani hakuna mwalimu ambaye anaipeleka timu uwanjani akifikiria kupoteza mchezo
wake.
“Kikubwa kilicho nyuma
ya mafanikio ni wachezaji kujitambua na kutimiza majukumu yao kwa wakati kwani
kila mchezaji ana kazi yake ndani ya uwanja ni suala la muda tu kupata matokeo
chanya," amesema.
Kagera Sugar ipo nafasi
ya pili ina pointi 22 ikiwa imecheza jumla ya mechi 10 ikipoteza mechi mbili na
kutoa sare mbili na imeshinda jumla ya mechi sita.







0 COMMENTS:
Post a Comment