Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, jana alijikuta akipewa ulinzi mkali na askari kufuatia kuzongwa na mashabiki wa klabu hiyo.
Aussems alijikuta akitaka kuzongwa na mashabiki ambao wengi wao walikuwa wakitaka kupiga naye picha sambamba na kutaka kumkumbatia.
Mashabiki hao baadhi walipiga kelele wakimtaka Kocha huyo aendelee kusalia ndani ya wekundu hao wa Msimbazi hata kama mabosi wake hawataki.
Walionekana kufurahishwa haswa na matokeo ya jana ambapo SImba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting.
Kumekuwa na tetesi kuwa Simba huenda ikaachana na Mbelgiji huyo huku ikielezwa miamba wa Polokwane City kutoka Afrika Kusini wakihitaji huduma yake.
Simba tusikurupuke aussems bonge la kocha
ReplyDelete