MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United Romelu Lukaku amesema kuwa aligundua kwamba haitajiki ndani ya kikosi hicho baada ya kubadilishiwa namba na kocha mkuu Ole Gunnar Solskajer alipokuwa ndani ya United.
Solskjaer aliamua kumtumia Anthony Martial ama Marcus Rashford kuwa washambuliaji halisi huku akimpangia Lukaku kuwa winga jambo ambalo lilikuwa linamfanya ashindwe kurejea kwenye ubora wake baada ya kuacha kucheza nafasi yake ya ushambuliaji.
Kwa sasa Lukaku raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26 amejiunga na Inter Milan inayoshiriki Serie A kwa ada ya pauni milioni 73 akitokea United inayoshiriki Ligi Kuu England na kesho itashuka uwanjani kumenyana na Sheffield.
“Nilikuwa na ndoto ya kujiunga na Inter Milan muda mrefu ili nicheze na Cristiano Ronaldo pamoja na Zlatan Ibrahimovic kwani nilijua huenda atarejea huku ila nilijua kwamba sina maisha marefu ndani ya United baada ya kuona nimebadilishiwa nafasi yangu ya asili kutoka mshambuliaji mpaka kuwa winga,” amesema.
2 Attachments
0 COMMENTS:
Post a Comment