MIRAJ
Athuman ‘Sheva’ mshambuliaji wa Simba amejipa kazi ngumu leo mbele ya Mbeya
City kwa kusema kuwa kama atashindwa kufunga bao akipata nafasi basi itampasa
atengeneza nafasi ya bao kwa mchezaji wake bila kujali nani atafunga.
Simba leo
itakuwa kazini ikimenyana na Mbeya City iliyo chini ya Kocha Mkuu Juma Mwambusi
uwanja wa Uhuru ambaye ana kumbukumbu ya kufutiwa kibarua chake na Simba msimu
uliopita wakati akiinoa Azam FC baada ya
kupoteza mchezo uwanja wa Taifa kwa kufungwa mabao 3-1.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Sheva amesema kuwa kwa sasa ligi imezidi kuwa ngumu kutokana na
ushindani uliopo jambo ambalo linawafanya nao wajipe kazi ngumu ya kufanya
ndani ya uwanja.
“Tulipoteza
mchezo wetu uliopita dhidi ya Mwadui tukiwa ugenini hilo tumeshasahau
tunajipanga kutafuta ushindi kwenye mchezo wetu mwingine, kilichobaki kwa sasa
ni kupambana kushinda kwenye mechi zetu zinazofuata.
“Kazi yangu
itakuwa moja tu kufunga endapo nitashindwa kufunga basi nyingine itakuwa ni
kutengeneza nafasi ya kufunga kwa wenzangu bila kujali nani atafunga kwani
kwenye mpira kinachotafutwa ni pointi tatu pekee,” amesema Sheva mwenye mabao
manne kwa sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment