LIVERPOOL KUMKOSA MCHEZAJI WAKE TEGEMEO KWA WIKI 10
KIUNGO tegemeo wa Liverpool, Fabinho anatarajiwa kukosa mechi kadhaa muhimu kwa timu yake kutokana na kupata majeraha ya kifundo cha mguu, aliumia katika mchezo juzi dhidi ya Napoli katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kiungo huyo Mbrazili amekuwa chaguo la kwanza chini ya Kocha Jurgen Klopp, alishindwa kuendelea na mchezo huo wa Napoli uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, hali ambayo imempa presha Klopp.
Fabinho hakufanyiwa vipimo Alhamisi kwa kuwa klabu ilitaka kuona akitulia kuona jeraha lake litaendelea kwa ukubwa gani, lakini baada ya kufanyiwa vipimo ikaonekana kuwa anatarajiwa kuwa nje kwa muda wa wiki sita.
Tangu kuanza kwa msimu huu Mbrazili huyo amekuwa akicheza nafasi kubwa kuhakikisha Liverpool inapata ushindi na kuongoza katika msimamo wa wa Premier League pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Ulaya.
Ikiwa itakuwa hivyo, inamaanisha kuwa atakosa michezo 10 ijayo ukiwemo dhidi ya Red Bull Salzburg katika Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na ile ya Klabu Bingwa Ulaya nchini Qatar.
Akizungumzia kumkosa mchezaji huyo, kiungo mwenzake Gini Wijnaldum alisema:
“Ni pigo kwa timu nzima lakini ni kitu ambacho tunatakiwa kupambana nacho.
0 COMMENTS:
Post a Comment