November 29, 2019


UONGOZI wa Klabu ya Yanga upo katika mchakato wa kutuma kikosi kazi kwa ajili ya kumfuatilia aliyekuwa kiungo wake, Haruna Niyonzima ambaye wanataka kumsajili kwenye dirisha dogo.

Niyonzima amekuwa kwenye kiwango cha juu kwa siku za hivi karibuni na mara ya mwisho alikuwa kwenye kikosi cha Simba ambapo aliachana nacho mwishoni mwa msimu uliopita.

Kwa sasa Niyonzima anakipiga katika Klabu ya AS Kigali ya Rwanda ambapo ameichezea kwa mafanikio makubwa timu yake hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amefunguka kuwa, kamati ya ufundi baada ya kukutana mwishoni mwa wiki iliyopita imekubaliana kumfuatilia Niyonzima kuona iwapo kiwango chake bado kipo vilevile ama la.

“Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji wanaoonekana kuhitajika sana ndani ya Yanga, kamati ya ufundi ya Yanga ilikutana wiki iliyopita na kuamua jambo moja la kumfuatilia kupitia mechi mbalimbali alizocheza na hata atakazocheza, tulidhani Rwanda itakuwa katika michuano ya Chalenji ili tuweze kupata nafasi ya kumchunguza lakini tumeona haipo.

“Kamati inahitaji kujua iwapo kiwango cha Niyonzima kinakidhi kuja kuichezea Yanga hii inayohitaji kuchukua ubingwa ama la, iwapo hatakuwa na kiwango basi tutaachana naye na iwapo kiwango chake kitairidhisha kamati ya ufundi basi tutamrejesha, hivyo kamati itatuma mtu wakati wowote kuanzia sasa, ijapokuwa sijajua ni nani ambaye atatumwa lakini tutatumia watu wengine ambao wapo kule.

“Yanga inahitaji kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu, kwani imedhamiria kweli kuweza kuwafurahisha mashabiki wake, ndiyo maana inahitaji kuwa na kikosi imara,” alisema Bumbuli.

Stori na Khadija Mngwai

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic