November 12, 2019


Na Lunyamadizo Mlyuka
SHOMARI Kapombe, mchezaji wa Timu ya Taifa anayekipiga timu ya Simba kwa sasa ambao ndio mabosi wake ameamua kwa hiyari yake yeye mwenyewe kuandika barua kuomba kustaafu kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania.

Kwa alichokifanya sio kitendo kibaya kwa kuwa ni maamuzi yake binafsi na hakuna ambaye amemlazimisha afanye jambo hilo ni wakati wake kutokana na maamuzi yake.

Hakuna ambaye hajui uwezo wa Kapombe akiwa ndani ya uwanja na kila mmoja kwenye ulimwengu wa mchezo anatambua thamani yake.

Kwa kuwa ameamua kufanya hivyo basi hapaswi kulaumiwa na wapenzi wa mpira kwa kudai kwamba ameisha muda wake ili hali bado ni kijana.

Ameandika barua ya kuomba kustaafu timu ya Taifa hiyo ipo wazi kutokana na dhamira yake kuona kwamba anahitaji kupumzika kuendelea na mambo yake ambayo ameyaweka bayana.

Tuheshimu maamuzi yake kwa kuwa kila mtanzania ana uhuru wa kuongea na kufanya kile ambacho anaona ni sahihi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.

Ameweka wazi sababu kubwa kuwa ni ile ya kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara hasa akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania.

Hilo lipo wazi kwani hata sasa bado anasumbuliwa na majeraha ambayo anayo na ikumbukwe kwamba mchezaji akiwa anapata majeraha ya mara kwa mara ufanisi wake unapungua.

Amekuwa hachezi mara kwa mara akiitwa timu ya Taifa kutokana na kusumbuliwa na majeraha hivyo ameomba apumzike ili apone majeraha yake.

Amekuwa anasumbuliwa na majeruhi kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likimfanya ashindwe kuitumikaia timu ya Taifa kipindi akiitwa.

Wakati wa michuano ya Chan pamoja na ile ya Kufuzu Kombe la Dunia alipata bahati ya kuitwa ndani ya timu ya Taifa.

Tukazungumza naye mengi kuhusu maisha ya soka na maisha binafsi, kiukweli aliongea mengi ambayo yanaumiza licha ya kwamba ni mpambanaji kwa sasa.

Alieleza hali halisi ya muda ambao anautumia kutibu majeraha yake kuwa mkubwa kuliko ule wa kuwa uwanjani jambo lililomfanya ashindwe kupata muda kuichezea timu ya Taifa.

Pia rekodi zinaonyesha kwamba majeraha yake mengi ameyapata timu ya taifa jambo hilo ndilo ambalo limemsukuma aombe kujiweka pembeni kwa muda.

Tuache kumdharau kwa maamuzi ambayo ameyafanya kwa sasa jukumu letu ni kuheshimu mawazo yake na kuendelea kumuombea ili arejee kwenye ubora wake.

Tusimbeze kwa kusema kuwa hana mchango ndani ya timu ya Taifa ana haki ya kuomba kile anachokiamini kutokana na hulka yake ya nidhamu.

Hakuna asiyependa kuitumkia timu ya taifa hasa kwa mzalendo mwenye utu na anayetambua kwamba ni heshima kuitumikia timu ya Taifa.

Umri wake bado mdogo unamruhusu kufanya mengi ambayo anayafikiria kwa sasa hivyo basi apewe nafasi ya kueleza kile kilicho ndani ya moyo wake.

Kwa kukaa kwake nje kutamfanya arejee kwenye ubora wake na wakati utafika atarejea kwenye ubora wake na ataomba kurejea kwenye timu ya Taifa.

Ushauri wangu kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inapaswa imuandalie mechi ya heshima kwa ajili ya kumpa sapoti na kutambua mchango wake ndani ya timu.

Kwa kufanya hivyo kutampa moyo Kapombe wa kuweza kurejea tena wakati afya yake itakaporejea kwenye ubora wake hasa kutokana na kuendelea kupambania afya yake.

Ipo siku atarejea kwenye uwanja na kuomba kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania ambayo ni ya kila mmoja kwenye kazi yake.

Wapenda soka tusisahau kumuombea Kapombe kwa kuwa tunatambua anapenda kuendelea kuitumikia timu yake ya Taifa ila majeraha ndio kikwazo kwake.

Imani ya wapenda soka ni kwamba atarejea na atapona majeraha yake ambayo yanamsumbua kwa sasa jambo litakalokuwa la furaha kwa wapenda soka.




2 COMMENTS:

  1. Kumuandalia mechi ni kupotea pesa zetu kwani ameahidi kurudi kuchezea timu hapo baadae cha msingi tusubiri isiwe sasa acheni mapenzi binafsi

    ReplyDelete
  2. HUWEZI KUMUANDALIA MECHI MCHEZAJI AMBAE ANAWEZA KURUDI KUICHEZEA TIMU YA TAIFA!!
    MCHEZAJI ANAYEANDALIWA MECHI NI YULE ANAYEAGWA MOJA KWA MOJA NA HATOWEZA TENA KUCHEZEA TIMU YA TAIFA !! NA KAMA NI HIVYO JIULIZENI JE WACHEZAJI WETU MAARUFU AMBAO WAMESTAAF SOKA MLIWAHI KUWAFANYIA AU HATA KUWAPIGIA DEBE!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic