DAVID Molinga, mshambuliaji wa Yanga, mibao yake anayofunga
kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara inafikirisha kutokana na aina yake na matokeo
ambayo timu yake inayapata.
Molinga amefunga mabao matatu katika Ligi Kuu Bara
ambayo yana rekodi yake huku mawili akiyafunga kwa mtindo mmoja na yote
amefunga Uwanja wa Uhuru.
Takwimu zinaonyesha kwamba akishafunga yeye hakuna
mchezaji mwingine wa Yanga anayefunga hadi mchezo unamalizika.
Bao lake la
kwanza alifunga Uhuru wakati Yanga ikilazimisha sare ya mabao 3-3 na Polisi
Tanzania ambapo alifunga akiwa ndani ya 18 kwa kichwa akimalizia pasi ya Mrisho
Ngassa na bao lake la pili alifunga kwa mpira wa adhabu uliozama moja kwa moja
ndani ya lango.
Bao lake la tatu alifunga juzi Uhuru mbele ya JKT Tanzania na Yanga
ilishinda mabao 3-2 na kusepa na pointi tatu jumla na bao lake alifunga kwa
mpira wa adhabu akiwa nje ya 18.
Kwenye mabao yake yote matatu, Molinga amekuwa
ni mkomelea nyundo wa mwisho kwa timu yake ya Yanga kwani akifunga kazi
inaishia hapo.
Yanga imecheza jumla ya mechi sita, imejikusanyia jumla ya
pointi 13, huku ikifunga mabao tisa, imefungwa mabao sita ikiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo.
0 COMMENTS:
Post a Comment