BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Hassan
Mwakinyo, leo Jumapili kwa mara ya kwanza atakutana uso kwa uso na mpinzani
wake, Mfilipino, Arnel Tinampay kwa lengo la kuelezea pambano lao
litakalofanyika Novemba 29, mwaka huu.
Mwakinyo na Tinampay wanakutana
leo kwenye viwanja vya Leaders kwa ajili ya kupima uzito na
kutambiana kuelekea katika pambano hilo litakalofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.
Hata hivyo, hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza kwa mabondia hao kukutana
uso kwa uso kabla ya pambano, lakini pia imeelezwa kuwa mabondia hao watafanyiwa vipimo vya kuwaangalia kama
hawatumii dawa za kusisimua misuli kabla ya kupanda
ulingoni.
Promota wa pambano
hilo, Juma Msangi, ‘Jay Msangi’ amesema kuwa mabondia hao watakutana
na amethibitisha Mwakinyo kutoa tiketi 500 kwa mashabiki wa
kwanza watakaofika uwanjani hapo.
“Mabondia wote watakutana kwenye viwanja vya
Leaders ili wakamilishe zoezi la kupima uzito na kutambiana wakiwa katika eneo
la wazi, lakini Mwakinyo ameahidi kutoa tiketi 500 kwa mashabiki 500 wa mwanzo
ili waweze kumuunga mkono katika pambano hilo,” amesema Msangi.
0 COMMENTS:
Post a Comment