Imeripotiwa kuwa Kocha wa Simba, Patrick Aussems tangu mechi ya Ruvu Shooting amesimamishwa kufanya kazi yoyote ndani ya klabu hiyo.
Taarifa imesema maamuzi hayo yamekuja kufuatia makosa mbalimbali aliyoyafanya Aussems ndani ya timu ikiwemo la kuondoka nchini bila ruhusa ya mabosi wake.
Mbali na kuondoka bila ruhusa, inaelezwa pia Aussems aligoma kukaa kitako na Ofisa Mtendaji wa klabu, Senzo Mazingisa ambacho kililenga kujadili mambo kadhaa kuhusu timu siku chache zilizopita.
Ukaichana na sababu tajwa hapo juu, inaelezwa pia kuwa uwezekano wa Aussems kuondoshwa ndani ya Simba upo kutokana na mwenendo wa kikosi cha timu ulivyo.
Inavyosemekana ni kuwa Aussems amekuwa na urafiki uliopitiliza na wachezaji kiasi cha kwanza inapelekea baadhi ya wachezaji kuwa na changamoto ya nidhamu jambo ambalo limechukuliwa kitofauti.
Sababu zote hizi ni nyepesi saana kumfukuza Kocha wa kariba ya Aussems. Ni juu ya Simba kutafakari kama huyu Mazingisa anaiongoza Simba kama klabu ya Mpira au Kiwanda cha nyembe?!
ReplyDeletewewe huna hata uelewa na unachoandika
Delete1.Senzo sio anayeajiri na kufukuza kocha hiyo ni kazi ya bodi.
2.Wewe unajua malengo ya Simba na mwenendo wa Simba kwa sasa kama vinaendana?
3.Aliyeajiri ndiye aliyefukuza sasa wewe kwa kuwa sababu zilimfanya akaajiri anazijua yeye na za kumfukuza anajua yeye kulingana na malengo ya timu
Maamuzi yatafikiwa na bodi na wala sio Mazingisa. Kama bodi itamuona ana hatia aondoke tu, hakuna namna nyingine. Huyu kocha ameshindwa kupandisha viwango vya wachezaji. Tumeona wachezaji waliokuwa kwenye viwango vya juu msimu uliopita wameporomoka sana. Mfani ni Tripple C Mwamba wa Lusaka. Kocha anawaachia wachezaji waende kulewa huku akijua kwamba ulevi utawashusha kiwango. Aende kwa amani, tunamshukuru kwa yale aliyoyafanya msimu uliopita. Kwa sasa hana jipya. Tunataka Simba yetu irudi kucheza mpira wa kasi kama ilivyo asili yake.
ReplyDeleteMlimuacha okwi mkasajiri magarasa sasa mnataka kumfukuza kocha mzuri tena mnataka nini nyinyi viongozi wetu nashindwa kuelewa baada ya kuangalia wachezaji wazuri tena washambuliaji kama okwi au zaidi tusajili sasa mnataka kumfukuza kocha kakosa nini? Mm ni mwanachama hai wa simba. Ningekuwa na namba ya MO ningemwambia huu upumbavu
ReplyDeleteJe mwenendo wa ulevi wa akina mkude,chama,wawa na wengine unauzungumziaje?
Deleteje kitendo cha kukataa wito wa CEO achilia mbali kuondoka bila kuaga nako unazungumziaje?
Masingisa anaivuruga simba
ReplyDeleteAussems hawezi kuondoka kwa sababu za kitoto kwa tujiulize mwenendo gani mbaya wa timu inayoongoza league? Acheni kupika Mambo Simba SC nguvu moja ni bland kubwa. Uongozi msifuate uchochezi wa wanahabari wachumia tumbo.
ReplyDeleteTeam zetu TZ subira ni kitu zinakosa...Sioni sababu za msingi za kumfukuza Aussems...labda kama amepatkana kocha bora zaidi yake...mafanikio uwanjani hayaji kwa msimu mmoja...
ReplyDelete