November 28, 2019


Ripoti kutoka Congo ambako klabu ya TP Mazembe inatokea zinasema kuwa miamba hao wa soka nchini humo na Afrika wapo kwenye mchakato wa kujenga uwanja mpya.

Inaelezwa uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza jumla ya watu ama zaidi ya watu 50,000.

Taarifa zinasema kuwa Rais wa klabu hiyo, Moyes Katumbi, ametangaza kuanza kuwa Mazembe itajenga kiwanja hicho ambacho kitakuwa ni moja ya viwanja vikubwa nchini Congo.

Maamuzi hayo yamekuja kufuatia Mazembe itakuwa inatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.

Maamuzi ya Mazembe ni sawa na wanachokifanya Simba kwa sasa ambao wanaelekea kukamilisha uwanja wa mazoezi kabla ya kuanza kujenga majukwaa hapo baadaye pamoja na Yanga ambao wameshaanza kuandaa uwanja wao Kigamboni, Dar es Salaam.

7 COMMENTS:

  1. Mazembe waige simba?huku tayari wana uwanja wao wanapanua kiwanja

    ReplyDelete
    Replies
    1. TP Mazembe wanao Uwanja wao wa michezo na wa mazoezi, una uwezo wa watazamaji 35,000.
      Huu mpya unakuwa na uwezo mkubwa zaidi, >50,000

      Delete
    2. Derrick,jenga tabia ya kujiridhisha kuhusu kile unachokipinga au kuunga mkono kabla ya kumshushua mtu ilhali huna unachokijua na matokeo yake unajiumbua wewe mwenyewe

      Stade TP Mazembe is a multi-use stadium located in the Kamalondo suburb of Lubumbashi, Democratic Republic of the Congo. Since its completion in 2011, it has mostly been used for football matches and is the home venue of TP Mazembe and CS Don Bosco. The stadium has 18,000 seats.

      Delete
  2. Kweli Mapenzi kitovu cha uzembe kazini... uwanja wa mazoezi ndio mazenbe wanataka kujenga leo???

    ReplyDelete
  3. Taarifa imekaa Kama vile TP Mazembe hawana uwanja. Hili sisawa. Ni ulinganisho mufilisi kabisa.

    ReplyDelete
  4. Mazembe mbona ni kama wana uwanja wao...ule wenye mamichoro michoro....hawawezi kuwa wanaiga simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic