November 11, 2019


Aliyekuwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, raia wa DR Congo, amesikia kelele za mashaibiki wa Simba wakitaka kocha wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems atimuliwe lakini akasema halitakuwa jambo zuri kwao lakini kama watafanya hivyo, basi wamchukue Florent Ibenge kwani ana uwezo wa kuwapa ubingwa wa Afrika.

Mashabiki wa Simba wameanza kupiga kelele wakidai Mbelgiji huyo ameishiwa mbinu kufuatia kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu dhidi ya UD Songo katika hatua ya awali kabla ya kufungwa na Mwadui kwenye Ligi Kuu Bara pamoja na sare dhidi ya Tanzania Prisons.

Zahera, ambaye ni kocha msaidizi wa DR Congo, ametoa ushauri huo ikiwa ni muda mchache baada ya kutimuliwa Yanga kwa kuwa aliweza kushuhudia mchezo wa Simba na Prisons kupitia runinga kabla ya kuelekea DR Congo kujiunga na timu ya taifa ya nchi hiyo inayojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon.

Ushauri wa Zahera umetokana na rekodi za Ibenge katika soka la Afrika akiwa na Klabu ya AS Vita ya DR Congo huku akiwa na kumbukumbu za kuwafunga Simba mabao matano kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Zahera alisema kuwa halitakuwa jambo jema kama Simba wataamua kumtimua kocha huyo lakini anaamini kama wakimchukua Ibenge atawabeba kutokana na kuwa na rekodi kubwa kwenye soka la Afrika.

“Niliona wakicheza na Prisons ambao walitoka nao sare, sasa mashabiki wao wameanza kupiga kelele kocha afukuzwe, imenishangaza kwa sababu hakuna timu inayoweza kushinda siku zote duniani hilo ni jambo la kawaida.

“Binafsi sioni haja ya wao kufanya hivyo na kama watafanya basi naweza kuwaambia wamchukue Ibenge yule wa AS Vita, namjua vizuri kutokana na rekodi zake, ana uwezo wa kuwapa hata ubingwa wa Afrika lakini haitakuwa suala rahisi kwao kutokana na bosi wa AS Vita kuwa na pesa nyingi kama ilivyo kwa Mo wa Simba,” alisema Zahera.

2 COMMENTS:

  1. Yaani unataka utuletee pacha wako aje kutuvuruga kama ulivyowavuruga vyura!!!!Hatuna akili za kushikiwa kihivyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic