PEP Guardiola,
Kocha Mkuu wa timu ya Manchester City amewashushia lawama waamuzi wote wa
mchezo wao wa Ligi Kuu England mbele ya Liverpool uliochezwa Anfield kwa kusema
kuwa umeegemea upande mmoja wa timu.
Mabingwa hao
watetezi wa Ligi Kuu England walishindwa kuivunja rekodi ya Liverpool kucheza
bila kufungwa kwa muda wa siku 900 wakiwa Anfield na kwa kupokea kichapo cha mabao
3-1 huku Guardiola akidai walistahili kupewa penalti mbili.
Mwamuzi wa
kati Michael Oliver ndiye ambaye alikuwa na jukumu la kuamua wapewe penalti au
la alipeta na kuwaruhusu kucheza jambo lililomfanya Guardiola raia wa Hispania avimbe kwa hasira na kumuonyesha ishara ya
vidole viwili mwamuzi wanne Mike Dean kumueleza hali halisi akidai Alexander Anorld
aligusa mpira.
Meneja wa
Liverpool, Jurgen Klop amesema kuwa hakuona kama kulikuwa na mazingira ya penalti
ila alishtushwa na goli la kwanza la mchezaji wake Fabinho kabla ya Mohamed Salah
kufunga bao la pili ambalo hajawahi kuliona kwa wachezaji wake ambao
walipambana kupata bao la tatu kupitia
kwa Sadio Mane.
City ilipata
bao kupitia kwa Bernardo Silva, ushindi huo unaifanya Liverpool kufikisha jumla
ya pointi 34 ikiwa nafasi ya kwanza huku City ikiachwa kwa jumla ya pointi 9
ikiwa na pointi 25 nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 12.
0 COMMENTS:
Post a Comment