MASOUD Djuma
aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa klabu ya Simba na kutwaa ubingwa kwa msimu wa
2017-18 akiwa na Mfarasa Pierre Lechantre inaelezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo
na uongozi wa klabu ya KMC ili kubeba mikoba ya Jackson Mayanja aliyefungashiwa
virago vyake klabuni hapo.
Mayanja alipewa
kandarasi ya mwaka mmoja iliyokuwa na kipengele cha kuongeza mkataba mwingine
iwapo atakidhi masharti yaliyowekwa kwa kufuata falsafa za klabu hiyo jambo
ambalo limekuwa gumu kwake kwa kile alichoeleza kutokuwa na washambuliaji
halisia ndani ya kikosi na amefungashiwa jumla virago.
Akizungumza
na Championi Jumatatu, Djuma alisema kuwa kwa sasa yupo nchini Rwanda
akiendelea na maisha yake kama kawaida kwani hana timu ya kufundisha baada ya
kuachana na AS Kigali.
“Kwa sasa
sina timu nipo naendelea na mambo yangu mwenyewe wakati ukifika nitajua jambo
la kufanya kwani nilishaachana na AS Kigali, suala la KMC kwa sasa sina taarifa
nalo ila kama itatokea tukafika maelewano nitafanya kazi kwani mimi ni kocha,”
alisema Djuma.
Ofisa Habari
wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa kwa sasa uongozi utaendelea na Kocha Mrage Kabange na Ahmady Ally mipango ya
kumpata kocha ipo chini ya uongozi wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment