November 12, 2019



SADIO Mane mshambuliaji wa Liverpool kwa sasa anazidi kutakata kwa kucheka na nyavu kwenye ligi Kuu ya England.

Mpaka sasa amecheza dakika 968 na amefunga jumla ya mabao 7 muhimu kwenye kikosi hicho kilicho chini ya Jurgen Klopp.

Ana wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 138 huku akitoa jumla ya pasi mbili za mwisho zilizoleta mabao.

Kinara wa utupiaji ni Jamie Vardy anayekipiga Leicester City ambaye ametupia jumla ya mabao 11 na pasi mbili za mwisho zilizoleta mabao.

Vardy ni Baba lao kwa sasa kwani amecheza jumla ya dakika 1080 huku akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 98.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic